MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo hadi hapo yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.
Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kujionea hali halisi ya kituo hicho.
Alisema
haiwezekani mawakala wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si
sahihi wakati katika eneo hilo hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya
maegesho ya magari.
“Nataka
maeneo rasmi yakishatengwa ndipo muanze kutoza faini, mmekuwa
mkiwasumbua wananchi hawajui wapi ni sehemu ya maegesho na wapi si
sehemu ya maegesho wekeni alama ndipo muanze kuwatoza,” alisema Makonda.
Licha
ya kutoa kauli hiyo, Makonda pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kabla ya
kumalizika wiki hii kuhakikisha kituo hicho kinawekwa taa ili kuondoa
usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi hasa wakati za usiku.
"Lakini
kabla ya wiki hii haijaisha nataka kuona taa zote za ubungo zinawaka,
sitaki kuviona vifusi katika eneo hili la stendi na baada ya siku 20
nitarejea kujionea utekelezaji wake kama umekamilika" Alisema Makonda
Katika
hatua nyingine, Makonda alisema kuwa serikali ipo katika mpango mwisho
wa kuihamishia stendi hiyo kutoka ubungo kwenda Mbezi mwisho.
"Shahuku
yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe
na stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo
halmashauri ya jiji tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo.
"Nataka
kuihamisha hii stendi ya ubungo ili tuepukane na kero ya kukutana na
mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote
maroli yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es
salaam maroli yanabeba ngano na makontena"
0 comments:
Post a Comment