Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Maalim Seif ahojiwa juu ya tuhuma za ufisadi.Fahamu zaidi hapa.
MAMLAKA ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA),
imemhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, baada ya kuwahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na tuhuma za ufisadi.
Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha ZAECA, Abubakari Mohamed Lunda,
alisema jana kuwa Maalim Seif alihojiwa na Mkurugenzi wa ZAEC, Mussa
Haji Ali, ili athibitishe tuhuma hizo.
Lunda alisema tuhuma zilizotolewa dhidi ya watendaji na viongozi ni
nzito ndiyo maana mamlaka hiyo imeamua kuchunguza ukweli wake kwa
manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.
Lunda alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuchunguza jambo lolote
ambalo linahusu maslahi ya Zanzibar katika kupambana na vitendo vya
rushwa na uhujumu uchumi.
“Tayari mamlaka imemhoji Maalim Seif ili kutafuta ukweli juu ya tuhuma
alizotoa za kuwapo viongozi wanaomiliki fedha chafu na mali nje ya
nchi,” alieleza Lunda.
Alisema nia ya kumhoji Maalim Seif ilikuwa kupata ukweli wa tuhuma
alizotoa dhidi ya viongozi na watendaji aliowatuhumu kwa kumiliki fedha
chafu na mali nje ya nchi.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>CCM Yakanusha Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete 'Kugoma' Kukabidhi Uenyekiti kwa Rais Magufuli.Fahamu zaidi hapa.
Baadhi
ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato
wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha
uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na des… Read More
#YALIYOJIRI>>>Hatma ya Bosi wa Zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya na wenzake Kujulikana Kesho Mahakama Kuu.Fahamu zaidi hapa.
Rufani
ya aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry
Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic
tawi la Tanzania ambaye pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996,
Shose… Read More
#YALIYOJIRI>>>Achinja Mke Na Mtoto Kisa Wivu Wa Mapenzi.Fahamu zaidi hapa.
JESHI
la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale (26) mkazi wa
Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuua kwa kuwachinja mkewe Oliver
Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana na wivu wa
map… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Mwita Waitara Azusha Tafrani Bungeni.Ni Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa.Fahamu zaidi hapa.
Mbunge
wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ametolewa nje ya Bunge baada ya
kutaka kumkwida Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agustine Holle (CCM) aliyedai
kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Kibamba… Read More
#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli Aongea na Wananchi wa Singida akiwa njiani kuelekea jijini Arusha kwa barabara.Fahamu zaidi hapa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiongea
na wananchi wa Mji wa Singida, wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani
kuelekea Jijini Arusha kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Dodoma,… Read More
0 comments:
Post a Comment