Majambazi
zaidi ya 15 yamevamia Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa
(Sekomu) kilichopo Kata ya Magamba, Lushoto mkoani Tanga na kuua mlinzi
mmoja, kumjeruhi mwingine baada ya kumpiga risasi begani, kuchoma
mabweni na kuharibu mali za wanafunzi waliokuwepo chuoni hapo.
Tukio
la majambazi hao kuvamia chuo hicho limetokea usiku wa kuamkia jana
wakati hali ya taharuki ikiwa bado haijasahaulika kwa wakazi wa Vikindu
wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani baada ya usiku wa kuamkia Ijumaa ya
wiki iliyopita Kikosi Maalumu cha Jeshi la Polisi cha Kupambana na
Uhalifu kupambana na genge la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi au
magaidi waliokuwa wakiishi katika nyumba iliyopo eneo hilo.
Wakati
tukio la chuoni hapo nalo likiibua shaka, hofu na maswali baada ya
majambazi hayo kutoiba chochote licha ya kutekeleza uhalifu huo, lile la
Vikundi ambalo msingi wake ulikuwa ni operesheni ya kuwasaka majambazi
waliowaua askari wanne wiki iliyopita waliokuwa wakibadilishana zamu ya
kulinda Tawi la Benki ya CRDB lililoko Mbande wilayani Temeke jijini Dar
es Salaam, likiwa limegubikwa na utata na sintofahamu huku Kamanda wa
Kikosi Maalumu cha Kuzuia Uhalifu, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Thomas Muniko, akiuawa kwa kupigwa risasi.
Licha
ya majambazi hayo kutekeleza tukio hilo baada ya kuvamia na kufunga
milango kwa nje na kumwaga mafuta na kuchoma moto mabweni huku baadhi ya
wanafunzi wakipiga kelele za kuomba msaada na wengine kufanikiwa kutoka
kupitia madirisha ya vyoo, lakini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Benedict Wakulyamba, amesisitiza kuwa kilichotokea chuoni hapo ni
ujambazi na si ugaidi.
Akizungumzia
tukio hilo jana kwa waandishi wa habari akiwa chuoni hapo, Wakulyamba,
alithibitisha kuwa lilihusisha majambazi kati ya 10 hadi 15 waliovamia
chuoni hapo na kuchoma vyumba vya mabweni mawili tofauti ya wanafunzi.
“Tukio
hilo ni la ujambazi na si ugaidi. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
itakaa kikao na kulijadili tukio hilo kisha tutatoa taarifa,” alisema.
Wakulyamba
alisema katika tukio hilo mlinzi mmoja wa chuo hicho, Yohana Shemzigwa
(34), aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito mgongoni na kichwani huku
mlinzi mwenzake, Abuu Rajabu, naye amejeruhiwa na majambazi hayo baada
ya kupigwa risasi begani.
Pia
alisema kuwa majambazi hayo yaliteketeza kwa moto mabweni mawili na
kusababisha magodoro, nguo na simu za viganjani za wanafunzi wa chuo
hicho kuungua.
Wakulyamba
alisema mmoja kati ya majambazi hayo alijeruhiwa vibaya wakati
akitekeleza unyama huo baada ya walinzi wa chuo hicho kutaka kumkamata
na amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto chini ya ulinzi wa
polisi huku akiwa mahututi.
Katika
hatua nyingine, alitangaza msako wa kuwasaka majambazi hayo ili
kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
“Niseme
kuwa sisi kama Jeshi la Polisi tutawatafuta wahusika wa tukio hili
popote walipo usiku na mchana, wawe mapangoni au nchi kavu lazima
tutawakamata na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria ili waweze kujibu
tuhuma zinazowakabili,” alisema Wakulyamba.
Tukio lilivyotokea
Akisimulia
tukio hilo jana mmoja kati ya wanafunzi wa chuo hicho, Elizabeth
Thobias, alisema lilitokea saa tano usiku wakati wakiwa mabwenini huku
wengine wakijiandaa kwenda kujisomea na kulazimika kutoroka ndani ya
mabweni hayo kwa kupitia madirisha ya vyoo.
Elizabeth
alisema majambazi hayo yalifika chuoni hapo saa nne usiku na kuanza
kuondoa vifaa vya kupoozea moto na kufunga milango kwa nje jambo
lililowapa wakati mgumu walipotaka kujiokoa.
“Majambazi
hayo yalipofika chuoni kabla ya kuanza kutekeleza ujambazi wao
walisikika wakijadiliana kwa kuambiana watuchinje kwanza au watuchome
moto, mmoja kati yao alisikika akisema moto tu unawatosha. Baada ya
kuanza kuchoma moto ndipo tukaanza kukimbilia na kujiokoa kupitia
madirisha ya vyoo vya mabweni,” alisema Elizabeth.
Tanga
imekumbwa na matukio kadhaa katika siku za nyuma likiwamo lililotokea
Februari, mwaka huu baada ya vikosi vya polisi na vile vya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupambana na majambazi yaliyojificha katika
Mapango ya Amboni na tukio jingine lilitokea Mei, mwaka huu baada ya
polisi kuwaua majambazi wanne walioweka kambi katika mapango hayo.
Pia
wakazi wengine wanane wa jijini Tanga walichinjwa na watu wasiojulikana
katika tukio lililotokea Juni, mwaka huu katika Kitongoji cha Kibatini
kilichopo Kata ya Mzizima
0 comments:
Post a Comment