Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi
mitaani hasa katika miji mikubwa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa
Jiji la Dar es salaam linaongoza kwa asilimia 28 ya watoto hao nchini
Hayo yamebainishwa leo Bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mhe
Khatib Said Haji Mbunge wa jimbo la Konde aliyetaka kujua serikali
inachukua hatua gani kukabiliana na ongezeko la watoto wa mtaani.
"Ni kweli kumekuwa na ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi
mitaani hasa katika miji mikubwa. Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika
katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza mwaka 2012 zilionesha kuwa Jiji
la Dar es Salaam lilikuwa na watoto 5,600 kutoka mikoa 10 ambayo ni Dar
es Salaam 28%, Dodoma 8%, Mwanza 7%, Morogoro 7%, Tanga 6%, Iringa 5%
Pwani 5%, Kilimanjaro 5% , Arusha 4%". Alisema Waziri Ummy
Aidha Waziri huyo amesema serikali ina jukumu la msingi la kuhakisha
ulinzi na usalama kwa watoto hao unapatikana pamoja na kushirikisha
jamii iweze kuwasaidia kuwaokoa vijana wanaoishi katika mazingira
hatarishi wakiwemo watoto wa mtaani.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment