Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya kutoa lugha chafu
inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliifuta kesi hiyo leo chini ya kifungu cha 225 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA).
Kesi hiyo imefutwa baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Maugo kueleza kuwa hawakuwa na shaidi na kuomba wapewe ahirisho.
Katika uendeshwaji wa kesi hiyo upande wa mashtaka uliita shahidi mmoja kwa miezi 14.
Katika
kesi hii, Gwajima anadaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25,2015 Tanganyika
Packers Kawe alitumia lugha chafu na kumdhihaki Muhadhama wa Kanisa
Katoliki Askofu Kardinal Polcarp Pengo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment