Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki alikamatwa April 5 usiku ambapo
taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa
studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake 4 na
wakapelekwa kusikojulikana.
Siku ya Ijumaa ya April 7, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda, aliahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili
watapatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu
wasiojulikana Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.
Alisema hayo akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda
mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo
kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.
Akiongea na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila
mtanzania ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna
anayejua watu hao wako wapi.
Mapema jana asubuhi kuhusu kutekwa kwa msanii huyo na wenzake,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro
alisema kuwa hawezi kusema ni lini wasanii hao watapatikana kwani ni
hadi pale upelelezi wanaouendesha utakapokamilika.
Sirro alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyekuwa
akiuliza kuhusu lini wasanii watapatikana kufuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa
aliyoitoa jana kuwa hadi Jumapili wasanii hao watakuwa wamepatikana.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana
lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye
Alisema Sirro
Mara baada ya tamko la Kamanda wa Polisi na Kabla ya Siku ya
Ijumapili (Leo), Wakina Roma waliripotiwa kuonekana kituo cha Polisi cha
OysterBay jijini humo.
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment