Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli leo
anatarajia kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya kisasa
(Standard Gauge) katika eneo la Pugu Jijini Dar es salaam.
Hayo
yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
alipotembelea eneo la mradi huo lililopo Pugu Jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa mradi huo utazalisha ajira nyingi katika kada mbalimbali.
Aidha,
aliongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utarahisisha usafiri wa kutoka
Dar es salaam hadi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Mwanza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli (RAHCO), Masanja
Kadogosa alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha shughuli
za usafiri na usafirishaji kwa kuwa safari ya Dar es salaam hadi
Morogoro itatumia muda wa saa 1:16, huku Dar es salaam hadi Dodoma
itatumia masaa 2:30 na safari ya Dar es salaam hadi Mwanza itatumia
masaa 7:30.
Mradi
huo ambao uko chini ya Kampuni za Merkezi ya Uturuki na Mota-Engil
Afrika ya Ureno, kwa awamu ya kwanza utaanza na kipande cha kilomita 300
kati ya Dar es salaam hadi Morogoro kwa gharama za dola bilioni moja za
Marekani.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment