Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbinga,
Leonard Kambo ambaye alidaiwa kuuawa na watu watano wa kanisa hilo
amekutwa akitoa ubatizo katika usharika wa KKKT Kitandilo, Makambako,
Mkoani Njombe.
Wakati
Mchungaji huyo aliyedaiwa kuuawa mwaka 2011 akionekana akitoa ubatizo
kanisani, watu waliodaiwa kumuua mchungaji huyo wamo mahabusu tangu
mwaka huo 2011.
Ndugu
wa watuhumiwa wa mauaji hayo ndio waliohaha kusaka picha ya mchungaji
huyo baada ya kupata taarifa kwamba alihamishiwa eneo la Makambako baada
ya kutokea tuhuma kwamba ameuawa.
Kwa
mujibu wa habari hizo, baada ya ndugu kupata taarifa kwamba mchungaji
huyo yupo hai, walitumia kila njia kupata picha yake ili itumike kama
ushahidi kwamba yupo hai na tuhuma dhidi ya wauaji si za kweli.
Muumini
mmoja wa kanisa hilo alieleza kuwa ndugu wa watuhumiwa hao
walihakikisha wanamnasa mchungaji huyo kwa kamera popote alipo ili
wasitishe kifungo cha ndugu zao na uongo dhidi yao.
Mmoja
wa watuhumiwa wa kesi hiyo ambaye alikamatwa kisha kuachiliwa huru,
Leonard Myale alisema kuwa baada ya kumuona na kupata picha ya mchungaji
huyo akiwa hai, watathibitisha Polisi ili akamatwe na watuhumiwa
wengine waachiwe huru.
“Tumeteswa
sana, tumedhalilishwa, tumepuuzwa na kusemwa vibaya na Wakristo
wenzetu, ndugu zetu na hata jamii haikutuamini juu ya tuhuma hizi za
uongo ambazo hata Polisi walitubambikiza kesi bila kufanya utafiti wa
kina. Tulikanusha kuhusika na mauaji hayo lakini Polisi hawakutuamini.
Sasa tunaamini tuko huru, wenye mamlaka watachukua hatua za kutusaidia” alisema Elenia Mhoka mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo.
Aidha
aliyewahi kuwa Mchungaji wa KKKT Kitandililo, Geofrey Mtweve,
alitafutwa ili kueleza kuhusiana na suala hilo, lakini hakutaka
kuzungumza chochote na kusema kuwa yeye siyo msemaji wa kanisa hilo.
“Mimi
si msemaji wa kanisa ila ni kweli nilikuwa Kitandililo, uongozi
umenihamisha kuja Ilembula, nimebadilishana na Mchungaji Leonard Kambo,
ambaye ndiye nimemkabidhi usharika, mengine sifahamu lolote. Wasiliana
na uongozi wa Jimbo,” alisema Mtweve.
Aidha
mchungaji Kambo alipotafutwa na kuulizwa kuhusiana na yeye kutuhumiwa
kifo na kama ni kweli aeleze kuwa alifufuka lini, lakini mawasiliano
yakawa mabovu.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, baada ya kuelezwa tukio hilo aliomba
kupatiwa picha na namba ya RB na kuahidi kuwa atalifanyia kazi suala
hilo.
Credit: TanzaniaDaima
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment