Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wa muungano huo baada ya kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.
February
27 2016 katika ukumbi wa Karimjee Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed
Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la
Ukonga, Mwita Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema,
mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya
Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu walidaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na
mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata mlalamikaji
Mmbando hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.
Aidha
ameongeza ushahidi wake ulielezea Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha
na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi, hivyo hakimu aliwaachia
huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment