Tuesday 27 September 2016

#BURUDANI>>>>Aunt Ezekiel Awajibu Wanaodai Anajipendekeza kwa Zari.Fahamu zaidi hapa.

Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Aunt Ezekiel amewamind mashabiki katika mitandao ya kijamii ambao wanadai anajipendekeza kwa mama watoto wa Diamond, Zari, baada ya hivi karibuni kuonekana akila nao bata pamoja.

Mwingizaji huyo ambaye alikuwa rafiki wa Wema Sepetu, amesema lazima awe karibu na familia ya bosi wa mume wake kwa kuwa hao ndio waliomwajiri mume wake.

“Nataka niwaambie kitu kimoja maana kujibu mmoja mmoja muda huo sina ni hivi nafanya nitakalo sifanyi mtakayo, maana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na mimi vibanda vya mbavu za mbwa vinawashinda, so muda mnaokaa mkafatilia yangu mngeenda kutafuta yakufanya, ooh! njaa yes i say tena yes maana 
mnataka nibadili red kuwa yellow kwani yule si ni boss wa mkata viuno wangu au!. Sasa kama ni bosi ulitaka nibishe niseme mimi ndio bosi, basi nifungue bendi yetu acheze!,” Aunt Ezekiel aliandika instagram.

Aliongeza, “Mnawazimu nini na namweshimu kama mshkaji rafiki bosi wa bwana yangu na siwezi acha kushirikiana na familia yake eti kisa ushuzi mtasema nini. Sitaki kutaja majina ya watu ila kilichopo ndio ukweli asilia, Mama Tee ndio mwanamke na mama watoto wa Nasibu no way hata tulambe lami kubadili ni ngumu ila mwenyewe akibadili basi na sisi tutabadili ila kwa sasa ni Mama tee shukrani gud Day,”.



Bongo5

0 comments:

Post a Comment