Home »
Habari Moto
» BREAKING NEWSMkuu wa Mkoa wa Arusha apiga marufuku uuzwaji kinywaji cha KIROBA.Fahamu zaidi hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.
Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata
ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za
kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira
ya kutatanisha.
Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa
serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa
serikali za mitaa.
Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi
wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki,
daladala na wapiga debe.
Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi,
amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua
za kisheria zitachukuliwa.
“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka
nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya
halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku
akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa
makini suala hili.”
Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na
ofisi za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au
kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za
vikao.
Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary
Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd
aliahidi kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>Magufuli Aitaka TRA Kutoa Mashine za EFDs Bure.Fahamu zaidi hapa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameishangaa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kutogawa bure Mashine za EFDs, na
wao kubaki na kazi ya kukusanya mapato.
Akizungumza
katika mkutano wa … Read More
#YALIYOJIRI>>>Gari la Magazeti ya Mwananchi Lapata Ajali....Wawili Wafariki Dunia Papo Hapo.fahamu zaidi hapa.
WATU
wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria
lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda
mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani
Ir… Read More
#Hivi Punde>>Waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim afanya Ziara nyingine ya kushtukiza ya katika bandari ya DSM na TRA.Fahamu zaidi hapa.
Ziara nyingine ya kushtukiza ya waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim katika bandari ya DSM na TRA yabaini upotevu wa makontena 2431.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015
… Read More
#YALIYOJIRI>>Watuhumiwa 8 wa Upotevu wa Makontena 349 Wafikishwa Mahakamani.Fahamu zaidi hapa.
WATUHUMIWA nane wa upotevu wa makontena 349 yaliyovushwa Bandarini ya
Dar es Salaam bila kulipiwa kodi, miongoni mwao akiwemo Kamishna wa Kodi
na Forodha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki
wamefikishwa kat… Read More
#YALIYOJIRI>>>Vigogo TRA Wakutwa na Mamilioni Nyumbani Kwao.Fahamu zaidi hapa.
Siku
chache baada ya kigogo mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
kubainika kumiliki nyumba 73, wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo
wamekutwa na mamilioni ya shilingi waliyoficha majumbani mwao.
Taarifa
… Read More
0 comments:
Post a Comment