Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (47) na
wenzake watatu leo wataendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Wakili wa Serikali Joseph Maugo alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu,
Godfrey Mwambapa kuwa kesi ilipangwa jana kwa ajili ya utetezi na wapo
tayari. Wakili mwingine wa Serikali katika shauri hilo ni Shadrack
Kimaro.
Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala na Faraja Mangula
ambao wote walikuwapo mahakamani jana lakini Hakimu Mfawidhi, Cyprian
Mkeha anayeisikiliza kesi hiyo hakuwapo.
Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi.
Katika kesi hiyo, Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali katika usalama.
\
Washtakiwa wenzake George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze
(39) na Georgey Milulu wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa
wakimiliki bastola aina ya Berretta na risasi 20 kinyume na sheria.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment