Serikali imesema kuwa hakuna mwekezaji yeyote aliyeruhusiwa kupewa
kibali cha kuingiza vifaranga au mayai ya kuku nchini kwa ajili ya
biashara.
Katika kusimamia hili, kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67,500 vilivyoingizwa nchini kinyume na sheria viliteketezwa.
Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvivu,
Mhe.William Ole Nasha amesema wapo wawekezaji wachache ambao hupewa
vibali maalum vya kuingiza mayai au vifaranga wa kuku wazazi (Parent
Stock) pekee na ukaguzi kwa ajili ya kudhibiti uingizaji vifaranga na
mayai unaendelea.
Amesema hatua kali zinachukuliwa kwa yeyote anayekamatwa kwa kukiuka utaratibu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment