Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Thomas Ngawaiya amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka
la kujenga hoteli kwa kutumia makandarasi wasiosajiliwa.
Ngawaiya
ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini na pia Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kilimanjaro, alipandishwa kizimbani jana na
kusomewa shtaka hilo, siku moja baada ya kutiwa mbaroni na Polisi
Kinondoni.
Kabla ya kumsomea shtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (ERB), Saddy Kambona alisema Ngawaiya
amefikishwa mahakamani hapo kwa kukaidi amri ya Mahakama.
Pia,
Wakili Kambona alimsomea mshtakiwa huyo shtaka linalomkabili, lakini
Ngawaiya alikana na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Wakili
Kambona alidai kuwa Machi 24, 2015 majira ya mchana, mshtakiwa alitenda
kosa la kuagiza ujenzi wa jengo la hoteli, kwa watu ambao
hawajasajiliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi.
Alidai kuwa
jengo hilo lipo Kiwanja Namba 32, makutano ya mitaa wa Dosi na Wazani,
eneo la Magomeni Mapipa, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aliendelea
kudai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu namba
22 cha Sheria ya Bodi Usajili wa Makandarasi, Namba 17 ya Mwaka 1997.
Akitoa
ufafanuzi nje ya Mahakama, Wakili Kambona alibainisha kuwa sheria hiyo
inamtaka kila anayejenga jengo ambalo ni kwa matumizi ya umma lazima
atumie makandarasi waliosajiliwa na ERB.
Baada ya kusomewa
shtaka hilo, kisha kuulizwa na Hakimu Hellen Liwa iwapo ni kweli au la,
Ngawaiya alianza kujitetea.
Hakimu Liwa alimzuia na kumtaka ajibu shtaka kabla ya Wakili wake, Desidery Ndibalema kuingilia kati na kumuelekeza kwa kumnong’oneza cha kufanya, ndipo akakanusha shtaka.
Hakimu Liwa alimzuia na kumtaka ajibu shtaka kabla ya Wakili wake, Desidery Ndibalema kuingilia kati na kumuelekeza kwa kumnong’oneza cha kufanya, ndipo akakanusha shtaka.
Wakili
Kambona baada ya kumsomea mshtakiwa shtaka hilo, alidai kuwa upelelezi
wa kesi hiyo unaendelea na kuomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa
ajili ya kutajwa. Hakimu Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili, 11.
0 comments:
Post a Comment