Home »
Habari Moto
» Diamond Amaliza ziara ya Ulaya, Adai Reality TV Show yake itaweka Wazi Mambo Mazito.Fahamu zaidi hapa.

Diamond Platnumz amemaliza ziara yake ya Ulaya aliyoipa jina, From
Tandale to The World Tour iliyompeleka kwenye nchi takriban nane.
Show yake ya mwisho ilifanyika Jumamosi hii jijini Copenhagen, Denmark ambayo video zake inaonesha ilikuwa na mafanikio makubwa.
Mchumba wake Zari aliyemsindikiza kwenye nchi zote alizopita, ameshukuru
kwa kuandika: Allow me to thank everyone that helped us while out there
in Europe. For showing us around and hosting us. Mostly thank you for
allowing my hubby entertain you. Stay blessed.
Tayari Zari amerejea Afrika Kusini kuungana na familia yake.
Katika hatua nyingine Diamond amedai kuwa reality TV show yake ijayo itaweka wazi mambo mengi mazito.
“Can you try to guess the name of our Reality Show?) (Muda si Mwingi
Kipindi cha Maisha yangu ya kila siku, Familia na Team yangu nzima
itaanza kuwa kwa Tv yako pendwa, ” ameandika Instagram.
“Nakuahidi sio tu eti Kireality show … ni Reality show Bora ambayo
naamini utaipenda kunzia kwenye Quality, Mikasa na matukio yote
nnayopitia mimi, Familia na Team yangu kila siku….Mengi yanaonekana,
Unayoyasikia, Unayasoma ila kwenye Hiki kipindi ndio itakuwa Thibitisho
la kila uvumi uusikiao….Sjui Kipini puani, Mara jicho, Mara sjui
@officialshetta , Mara DNA, Mara @romyjons kutoinekana tena kwenye Tour
Ghafla….Niamini mimi yote utaona na kuyapata kwa uwazi kabisa, Kaa na
Mimi…….! We unavyohisi reality Show yetu itakuwa inaitwaje…..?”
ameongeza
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>DARAJA LA KIGAMBONI KUFUNGULIWA RASMI APRILI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata
maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni
Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es salaam.
… Read More
#YALIYOJIRI>>>SERIKALI YAIPANDISHA ZAHANATI YA MSOGA KUWA HOSPITALI YA WILAYA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya
Msoga, Dk. Juliet Lema wakati wa ukaguzi huo. Kulia ni Mganga Mkuu wa
Mkoa … Read More
#YALIYOJIRI>>> SAFARI ZA TRENI RELI YA KATI ZAANZA RASMI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Huduma
ya usafiri wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi
miwili sasa imerejea kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo
katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogor… Read More
#YALIYOJIRI>>>Lowassa Afunguka Mazito Kuhusu Wanachama Wanaofukuzwa CCM Wakituhumiwa Kukisaliti Chama Kwa Kumuunga Mkono Yeye.Fahamu zaidi hapa.
Aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Edward Lowassa amewapa neno wanachama wa CCM wanaotaka
kufukuzwa ndani ya chama hicho wakituhumiwa kumuunga mkono.
Akiongea
hivi k… Read More
#YALIYOJIRI>>>Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka Ashitakiwa Tena Kwa Uhujumu Uchumi.Fahamu zaidi hapa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka
na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka sita
yakiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kuisababishia… Read More
0 comments:
Post a Comment