Mfanyabiashara
maarufu wa kiarabu Dk Sulaiman Al-Fahim ametangazwa kuwa mwenyekiti
mtendaji wa klabu ya African Lyon ambayo itashiriki ligi kuu ya Tanzania
Bara msimu ujao.
Mmiliki
wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi alisema kuwa waliamua kumuomba
Al Fahim kuwa kushika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake katika michezo
hasa mpira wa miguu mbali ya kuwa mfanyabiashara bilionea katika nchi
za Uarabuni na duniani kwa ujumla.
Kangezi
alisema kuwa Al Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate
Development ya Dubai na miaka ya nyuma alikuwa msemaji wa kampuni
inayomiliki klabu tajiri duniani, Manchester City, Abu Dhabi United
Group (ADUG). ADUG ilinunua Manchester City mwaka Septemba, 2008.
Pia
Al Fahim alitaka kununua klabu ya Portsmouth ambayo ilikuwa inashiriki
ligi kuu ya Uingereza, lakini mpango huo haukuweza kukamilika.
Kangezi
alisema kuwa Al Fahim ataanza kazi rasmi Aprili 16 ambapo atatangaza
timu yake ambayo atafanya nayo kazi katika kuibadili klabu hiyo na kuwa
klabu bora Tanzania na Bara la Afrika.
Alisema
kuwa uwepo wa Al Fahim kuitaifanya timu hiyo kuwa na uongozi bora wenye
kujua uendeshaji wa kisasa katika masuala ya mpira kwa kuzingatia
uzoefu wa mfanya biashara huyo mzoefu katika soka na michezo
mengine.“Haikuwa kazi rahisi Al Fahim kukubali kuingia kwenye uongozi
wa klabu yetu, ila tunashukuru kwani alituelewa baada ya kukutana naye
alipokuja hapa nchini kwa shughuli zake, “ alisema Kangezi.
Alisema
kuwa lengo lake ni kuona African Lyon inakuwa klabu ya mfano sit u kwa
Tanzania, hata kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Kangezi alisema kuwa mipango yao ya awali ni kuhimarisha timu ya kwanza
ili iweze kufanya vyema katika mashindano ya ligi kuu na pia kuanzisha
msingi mzuri wa timu za watoto.
“Dk
Sulaiman ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Al Fahim Group na
vile vile alikuwa mkurugenzi wa kituo cha Royal Football Fund (RFF)
mbali ya kuwa mchezaji wa mchezo wa chesi, ameahidi kusaidia wachezaji
chipukizi ili kuwawezesha kushiriki katika mpira wa kulipwa, tunaamini
titafika, ” alisema.
0 comments:
Post a Comment