Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Bulembo: Lowassa ni Fisadi, Namshauri Amwache Rais Magufuli na Badala yake Aende Kijijini Kuchunga Ng'ombe.Fahamu zaidi hapa.

Mwenyekiti
wa Jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo
amemtaka waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amwache Rais Magufuli
aendelee kufanya kazi zake.
Bulembo
anakuwa kiongozi wa pili wa CCM kumvaa Lowassa aliyekosoa utendaji wa
Rais Magufuli wa kutumbua majipu wakati alipokutana na wanazuoni wa
ndani na nje ya nje Alhamisi ya wiki hii, baada ya juzi msemaji wa CCM
Christopher Ole Sendeka naye kumkosoa kuwa si kweli kwamba watumishi
wa umma wanafukuzwa bila kusikilizwa.
Akizungumza
mjini hapa jana na wanachama wenzake wakati wa maadhimisho ya miaka
61 ya Jumuiya hiyo yaliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro, Bulembo
alimtaka Lowassa kutekeleza ahadi yake ya kwenda Monduli kuchunga
ng'ombe kama hatochaguliwa kuwa Rais.
"Kama
yeye anasema kasi ya Magufuli ni ya muda au anakosea kutumbua majipu,
basi tunamkumbusha kauli yake wakati akiongea na vyombo vya habari kuwa
akishindwa urais atarudi kijijini kwake kuchunga ng'ombe, tunaomba
aende akafanye kazi aliyoahidi. " Alisema Bulembo.
Alisema
anashangazwa na Liwassa aliyekuwa mgombea urais mwaka jana kupitia
Chadema chini ya mwamvuli wa UKAWA kusema ndani ya CCM kumejaa ufisadi
wakati yeye ni fisadi namba moja.
Katika hatua nyingine, Bulembo alisema ndani ya CCM kuna majipu yanayohitaji kutumbuliwa wakiwemo Wasaliti.
Alisema wanasubiri Rais Magufuli akabidhiwe uenyekiti wa CCM mwezi wa saba mwaka huu ili waanze kuyatumbua majipu hayo.
Related Posts:
AFUNGWA Jela Maisha Kwa Kuiba Simu ya Sh 110,000 na Kujeruhi.Fahamu zaidi hapa.
Kesi ya wizi wa simu aina ya Tecno iliyochukua takriban miaka miwili
mahakamani, imefika tamati kwa mtuhumiwa kufungwa maisha jela.
Hukumu hiyo ilifikiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya
mtuhumiwa Kassim… Read More
#BREAKING NEWS>>>>BASI LA ABIRIA LAPATA AJALI SINGIDA MUDA HUU.FAHAMU ZAIDI HAPA.
zinasemekana kwamba watu watatu wamefariki dunia akiwemo Dereva wa bus hilo
Katika maelezo niliyo yapata mke wa Dereva nae alikuwa ndani ya hilo bus ila yey kasalimika.
Lakini amemlilia mume wake mno baad… Read More
HII ndiyo Simu ya Milioni 16.5 Anayotumia Bilionea Alhaj Dangote.Fahamu zaidi hapa.
Inasemekana hii ndio simu anayotumia Bilionea Alahaji Aliko Dangote.
Inaitwa Nokia Vertu Signature. Bei yake ni kati ya $5000 hadi $7500.
Ukibadilisha kwa pesa ya madafu ni kama milioni 16.5Tsh hivi. Alhaji sio
mtu wa ki… Read More
Urusi Yaapa Kulipiza Kisasi Baada ya Marekani Kuwatimua Wanadiplomasia wa Urusi.Fahamu zaidi hapa.
Urusi
imeonya kwamba italipiza kisasi hatua ya rais wa Marekani Barrack Obama
ya kuwatimua wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma kwamba Urusi
iliingilia maswala ya uchaguzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa
mitan… Read More
ALIYECHOMWA MKUKI MDOMONI ASIMULIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
MKAZI wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata
ya Masanze, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, Augustino Mtitu,
aliyechomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni, amemshukuru Mungu,
madaktari, uongozi wa ha… Read More
0 comments:
Post a Comment