Hatimaye
hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Saed Kubenea, Mbunge
wa Jimbo la Ubungo akidaiwa kumtolea lugha ya matusi Paul Makonda, Mkuu
wa Wilaya ya Kindononi imefika tamati.
Thomas
Simba, Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es
Salaam amesema, mahakama hiyo imemtia hatiani Kubenea na kumpa adhabu ya
kutofanya kosa linalofanana na hilo ndani ya miezi mitatu.
“Mahakama
imejiridhisha kuwa, hilo ni kosa lako la kwanza na kwa kuzingatia nia
uliyoenda nayo ya kutatua mgogoro wa wafanyakazi, lakini pia
imejiridhisha kwa kutumia ushahidi wa upande wa mashtaka, hivyo
inakutaka usifanye kosa linalofanana na hilo na kuletwa tena
mahakamani” amesema hakimu.
Amesema
kuwa, kila upande upo huru kukata rufaa endapo wataona kuwa hukumu
iliyotolewa hawaridhiki nayo, ambapo pale pale jopo la mawakili wa
Kubenea likiongozwa na Peter Kibatala, waliiambia mahakama kuwa wanaweka
nia ya kukata rufaa kwa sababu ushahidi uliotumika kuhukumu umeacha
mashaka mengi.
Nje
ya mahakama Kubenea amewaambia waandishi wa habari kuwa yeye bado ni
Mbunge wa Ubungo na wananchi wa Ubungo wasiwe na hofu kwani hizo ni
harakati za siasa.
John
Mallya, mmoja wa mawakili aliyekuwa akimtetea Kubenea amesema kuwa,
mahakama haikupaswa kuegemea kwenye ushahidi wa polisi peke yake
kufikia uamuzi huo kwa kuwa polisi wasingeweza kumpinga Makonda.
Amehoji ni kwanini upande wa Jamhuri haukuleta mfanyakazi hata mmoja kutoa ushahidi.
Kesi
hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi hao
wawili kutofautina kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo,
jijini Dar es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana ambapo Kubenea
alikamatwa na polisi kwenye eneo hilo kwa amri Makonda.
Tukio
hilo lilitokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda
hicho ambao walimpigia mbunge huyo aende kutatua mgogoro huo.
Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana na kukutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.
Ilipofika
saa 10:30, Makonda alifika na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa
kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.
Alitoa
amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri
wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya
Wanawake, Jinsia na Watoto.
Baada
ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Kubenea kuhutubia na kuaga
wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo (Kubenea)
alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.
Makonda
alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo,
alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea ambapo sintofahamu
iliongezeka.
<a
href='http://mpekuzihosting.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a5fa0220&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE'
target='_blank'><img alt='' border='0'
src='http://mpekuzihosting.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=3&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE&n=a5fa0220'/></a>
0 comments:
Post a Comment