Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri
ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais
kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.
Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa
tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii.
Muungano wa vyama kadha vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea mwezi MachiBw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo ni za uongo.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.
0 comments:
Post a Comment