Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa
uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati. Hii ni
kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa – IMF.
Katika ripoti yake iliyotolewa jana Tanzania inatarajiwa kusajili
kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka 2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya
Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .Ivory Coast
inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.
IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa
jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo
kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa – IMF, eneo hilo
linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka
huu.Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka
15.
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo
yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola. Aidha Zambia pia
imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba
yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha
ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
- Ivory Coast 8.5%
- Tanzania 6.9%
- Senegal 6.6%
- Kenya 6%
- Zambia 3.4%
- Nigeria 2.3%
- Afrika Kusini 0.6%
0 comments:
Post a Comment