Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetoa onyo pamoja na kuutaka uongozi wa Clouds TV kuomba radhi Watanzania kupitia taarifa zake za habari ndani ya siku tano mfululizo kuanzia leo.

Adhabu hiyo imetolewa leo na kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), baada ya baadhi ya wananchi hususani watazamaji wa kipindi cha ‘Take One’ kilichorushwa 28 Juni mwaka huu ambacho kilidaiwa kurusha hewani kipindi hicho kilichozungumzia masuala ya mapenzi ya jinsia moja (Ushoga) na hivyo kulalamikiwa na wananchi kwamba kwamba kilikiuka maadili ya taifa kwani kipindi hicho  kiliwakwaza pamoja na kuwasababishia usumbufu wananchi hususani watazamaji kwa kuwasilisha mada inayozungumzia masuala ya mapenzi ya jinsia moja (ushoga),

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Joseph Mapunda amesema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wajumbe wa kamati kutafakari maelezo ya utetezi yaliyotolewa na uongozi wa Clouds TV.