Simba
ipo kambini mkoani Morogoro ikijiandaa na msimu ujao wa 2016/17, lakini
habari nzuri ni kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog anaonekana
kuwa ‘serious’ na kazi yake, ndiyo maana akaamua kikosi chake
kikajifiche nje ya mji mkoani hapa.
Championi
Ijumaa ambalo ni gazeti pekee kufika kwenye kambi hiyo iliyopo eneo la
Highlands ambapo kuna taasisi ya dini, imeshuhudia mchakato
unavyoendelea ambapo sura za wachezaji wa timu hiyo zinaonekana kuwa
katika hali ya furaha na kufurahia kile ambacho wanaelekezwa na benchi
lao la ufundi.
Katika
mazoezi ya jana asubuhi, Simba ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwa
misimu minne mfululizo, wachezaji wake hawakuwa na kazi kubwa ya
kufanya, Omog alionekana akitoa maelekezo zaidi kuliko wachezaji kucheza
mpira huku utulivu wa mazingira ukionekana kuwa wa kiwango cha juu kama
vile timu ipo Ulaya ambapo kunasifika kuwa na sehemu nzuri tulivu na
zenye viwanja bora vya mazoezi.
Saa
2:30 asubuhi ratiba ilianza kwa wachezaji wa Simba kufika uwanjani
wakitokea kwenye vyumba ambavyo vipo eneo hilohilo, walifika na kuanza
mazoezi ya viungo.
Baadaye
wakaanza kuruka koni, walipomaliza hapo wakaanza kuuchezea mpira
kidogo, kisha wakawa wanapiga mpira kwa vichwa katika staili ya
kuonyesha uwezo wao wa kumiliki mpira.
Baada
ya hapo wakarushiana mpira kwa muda kidogo, kisha wakakusanyika
katikati wakaanza kunyoosha viungo na kuanza kupewa maelekezo muhimu na
Omog.
Omog
alichukua muda mrefu kudogo kutoa maelezo huku akishirikiana na
msaidizi wake, Jackson Mayanja raia wa Uganda. baada ya hapo wakaondoka
na kurejea kambini.
Mazingira
ya kambi hiyo ni mazuri, nyasi za uwanja wanaofanyia mazoezi ni nzuri
na zenye kiwango bora, pia kuna hali ya utulivu na kila mmoja ambaye
anakuwepo mazoezini anaonekana kufanya majukumu yake bila kufokewa wala
kupigiana kelele akiwemo daktari wa timu hiyo, Yasini Gembe.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment