ABAJALO.
Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti, Richard
Sinamtwa imebaini kasoro kwa Abajalo FC kumtumia mchezaji Laurent E.
Mugia hivyo kuamua kumfungia mchezaji huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja
kwa mujibu wa kanuni ya 36 (16) toleo la mwaka 2014 la Ligi Daraja la
Pili kwa kosa la kuchezea klabu mbili katika msimu mmoja.
Kwa
kuwa kanuni za Ligi Daraja la Pili mpaka Ligi Kuu zina upungufu
unaofanyiwa mapitio pale kiongozi wa timu anapofanya udanganyifu wa
usajili wa mchezaji bila kumshirikisha mchezaji, Kamati sasa imelazimika
kutumia kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ibara ya
VII (10) ikinukuu:
“A
team which will have committed a fraud on the identity of player or
which will have allowed a suspended or non-qualified player to take part
in match shall, lose the match and shall be completely eliminated from
the competition as soon as the incriminating fact are clearly
established by CAF organizing committee.” Mwisho wa kunukuu.
Kwa
maelezo hayo, timu ya Abajalo FC inanyang’anywa pointi sita. Timu za
Pamba SC na The Mighty Elephant wanapewa pointi tatu kila timu na magoli
matatu.
Kamati
inaagiza Sektretarieti kuwachukulia hatua na kuwapeleka katika vyombo
vya Serikali viongozi wote wa timu ya Abajalo walioshiriki kubadilisha
jina la mchezaji alilotumia akiwa na timu ya Kagera Sugar ili
kufanikisha usajili wao na pia kwa kubadilisha tarehe, mwezi na mwaka wa
kuzaliwa za mchezaji ili kufanikisha usajili wao kwa msingi kwamba
waligushi.
Uamuzi
huu, ni wa mwisho na kwamba kama kuna ambaye hajaridhika, ana nafasi ya
kukata rufaa kwenye CAS - Mahakama ya Mashauri ya Soka ya FIFA iliyoko
Geneva, Uswisi.
Awali
kwa nyakati tofauti, Pamba SC ya Mwanza na The Mighty Elephant ya
Songea zilikata rufaa kuilalamikia Abajalo FC kwa kumtumia mchezaji wa
Kaliua City ya Tabora, Laurence Mugia kutoka Kagera Sugar katika michezo
ya mtoano wa Ligi Daraja la Pili kwa ajili ya kupanda daraja la kwanzaa
huku wakijua kuwa ni kosa kwa mujibu wa kanuni.
0 comments:
Post a Comment