Friday 8 July 2016

#MICHEZO>>>>Kocha kuu wa timu ya Mtibwa Sugar Maxime ameihama Mtibwa Sugar.Fahamu zaidi hapa.

Mecky Maxime amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha klabu ya Kagera Sugar baada ya klabu  kuachana na kocha wao Adolf Rishard aliyemalizia raundi ya pili ya VPL msimu wa 2015-16.

Uongozi wa Kagera Sugar umesema umevutiwa na Maxime kutokana na mwendelezo wake wa matokeo mazuri akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar lakini wakaongeza kwamba wao ni waumini wa makocha wazawa.
Msimu uliopita Mexime aliisadia Mtibwa kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa VPL kati ya timu 16. Mtibwa ilimaliza kikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 30, ikiwa imepata ushindi katika mechi 14, sare 8 na kupoteza mechi 8.

0 comments:

Post a Comment