WAZIRI
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amekuwa miongoni mwa mamia ya
waombolezaji walioshiriki maziko ya mbunge wa zamani, Beatrice
Shelukindo (58) yaliyofanyika nyumbani kwa wazazi wake katika kata ya
Olorien Jijini Arusha jana.
Viongozi
wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyotanguliwa na ibada ni pamoja na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu, Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani, Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Felix Ntibenda.
Pia
maziko hayo yalihudhuriwa na wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Tanga na Arusha, Meya wa Halmashauri
ya Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro na viongozi wengine wa vyama vya siasa
na serikali.
Ibada
ilifanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana, Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro ambako Askofu mstaafu, Simon Makundi, alisema Beatrice
hakuwa fisadi na alitoa mchango mkubwa kwa familia, dini, taifa na
Afrika Mashariki.
“Jiulize wewe una mchango gani hata katika familia yako, dini yako, taifa hili na hata kwa Afrika Mashariki?” Alihoji Makundi.
Aliwataka
mamia ya waombolezaji wakipewa nafasi, heshima na vyeo serikalini au
katika kampuni yo yote kuitunza heshima hiyo kwa kufanya kazi kwa
uadilifu na kuwa na hofu ya Mungu.
Beatrice aliyezaliwa mwaka 1958 amefariki akiwa na umri wa miaka 58, jambo ambalo askofu mstaafu alisema hiyo ni neema ya Mungu.
0 comments:
Post a Comment