Friday 8 July 2016

Ben Pol asema yeye ndo anachelewesha kufanyika kwa kolabo yake na Diamond.Fahamu zaidi hapa.

Hit maker wa ‘Moyo Mashine’ Ben Pol amesema tayari ameshazungumza na uongozi wa Diamond Platnumz kuhusu kufanya kolabo na staa huyo wa wimbo ‘Utanipenda’.

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Ben Pol amesema muda wowote kuanzia sasa anaweza kuingia studio na staa huyo.

“Nataka kufanya kazi na Diamond na nimeshaongea nao ila mimi ndo nachelewesha hii kazi,” alisema Ben Pol.

Muimbaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania ambao wanafanya vizuri kimataifa, Jumapili hii atakuwa na ‘Moyo Mashine Night’ itayofanyika Maisha Masement.

0 comments:

Post a Comment