Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.
Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.
Mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema amesema maafisa wa polisi bado wanakabiliana na mshukiwa mmoja ambaye anadaiwa kujibanza katika jumba linalotumiwa kuegesha magari.
“Mshukiwa huyo ambaye tunawasiliana naye amewaambia maafisa wetu kwamba mwisho unakaribia na kwamba ataumiza na kuua wenzetu wengi, akimaanisha maafisa wa usalama na kwamba kuna mabomu yaliyotegwa eneo lote, kwenye gereji na katikati mwa jiji.”
Vyombo vya habari jimbo hilo vinasema kumetokea mlipuko mkubwa eneo hilo lakini habari hizo hazijathibitishwa.
- Mtu mweusi Sterling alivyouawa Marekani
Waliuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya weusi.
Takwimu kutoka kwa shirika linalotetea maafisa wa polisi Marekani la Officer Down Memorial zinaonesha maafisa 53 wa polisi wameuawa wakiwa kazini mwaka 2016, 21 wakiuawa kwa kupigwa risasi. Idadi hiyo haijumuishi maafisa waliouawa Dallas.
Ufyatuaji risasi ulitokea mwendo wa saa tatu kasorobo usiku saa za Texas waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.
Maandamano hayo yalitokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge jimbo la Louisiana.
Miongoni mwa maafisa wa polisi waliofariki ni afisa wa trafiki Brent Thompson, 43.
- Donald Trump anusurika kuuawa
Meya wa Dallas Mike Rawlings amesema "huu ni wakati wa kusikitisha sana kwa jiji letu.”
Rais wa Marekani Barack Obama, akirejelea takwimu zinazoonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Wamarekani Weusi kupigwa risasi na maafisa wa polisi kuliko Wamarekani Wazungu, amesema ubaguzi huo unafaa kumalizwa.
Waliuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya weusi
Takwimu kutoka kwa shirika linalotetea maafisa wa polisi Marekani la Officer Down Memorial zinaonesha maafisa 53 wa polisi wameuawa wakiwa kazini mwaka 2016, 21 wakiuawa kwa kupigwa risasi. Idadi hiyo haijumuishi maafisa waliouawa
Dallas.
Chanzo BBC SWAHILI.
0 comments:
Post a Comment