Saturday 9 July 2016

#YALIYOJIRI>>>Picha: Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu) alivyonyanyua kidole cha kati akiwa bungeni.Fahamu zaidi hapa.

Picha hii ikimuonyesha Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbili maarufu kama Sugu akinyanyua kidole cha kati juu alipokuwa akitoka bungeni wakati wa vikao vya Bunge mjini Dodoma mwezi Juni.
Kufuatia kitendo hicho Joseph Mbilinyi alisimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya Bunge kuanzi Juni 30.
Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kile alichoeleza kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake. 

Hata hivyo alipohojiwa kama anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi alisema kuwa hamfahamu.

0 comments:

Post a Comment