Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa
(mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa
utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.
Mkuu
wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo
visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya
watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni
kinyume na maadili ya mtanzania.
Aidha
alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya
jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha
anawamaliza wote mkoani
Sakati
hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya
kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii
ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na
kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.
0 comments:
Post a Comment