Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kampuni ya udalali ya Yono
Auction Mart & Co imeifungia kampuni ya Mkono & Company Advocate
kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya kodi inayofikia Sh1 bilioni.
Kampuni hiyo inahusishwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM) ambaye pia ni wakili maarufu nchini.
Kampuni hiyo inahusishwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM) ambaye pia ni wakili maarufu nchini.
Hata
hivyo, Mkono
hakupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo. Hati ya TRA iliyosainiwa
na Kamishna wa TRA, Neema Mrema imesema Yono imepewa mamlaka na
Kamishina Mkuu wa mamlaka hiyo chini ya kifungu cha 64 cha Sheria ya
Kodi ya mwaka 2015 ya kushika mali za mdaiwa anayeshindwa kulipa kodi.
“Naomba kupata usaidizi wa Yono Auction Mart & Company Ltd na
Polisi kutaifisha na kuhamisha bidhaa na mali popote zilipo ili kwa njia
yoyote zikiuzwa zilipe deni jumla ya Sh1,101,432,045.99 pamoja na
gharama za wito uliotolewa chini ya Kamishna….” ilisema sehemu ya hati
hiyo.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Yono Auction Mart Co.
Ltd, Stanley Yono alikiri kuifungia kampuni hiyo mpaka itakapolipa deni
hilo.
“Ni kweli tumeifungia kampuni ya uwakili ya Mkono na hapa tuko
kwenye eneo la tukio. Anadaiwa zaidi ya Sh1 bilioni ikiwa ni malimbikizo
ya VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani), kodi za mishahara na nyinginezo
kwa mwaka mzima. Amegoma kutia saini hii hati lakini haitasaidia kitu
kwani tumeshamfungia,” alisema Yono.
0 comments:
Post a Comment