UMOJA wa Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), umeapa kutotoa ushirikiano wa kikazi kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioteuliwa na Rais John Magufuli ambao wanatoa matamko yasiyo na tija kwa wananchi.
Mkuu
wa Idara ya Habari na Uenezi wa JUVICUF, Dahlia Majid alisema katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa uteuzi wa makada
wa CCM katika nafasi za wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi utavuruga
nchi hususani katika kipindi cha uchaguzi.
Akisoma
tamko hilo kwa niaba ya Mwenyekiti wa JUVICUF Taifa, Hamidu Bobali,
Dahlia alisema viongozi wa awamu ya tano wanakurupuka na kutoa matamko
yasiyo na tija yanayobaka mamlaka ya Jeshi la Polisi.
“Haiwezekani
viongozi wa awamu ya tano wanakurupuka tu wanatoa matamko yasiyo na
tija kila siku tena mengine yanabaka mamlaka hata ya mahakama na
wanajifanya wao ndio polisi, wao ndio mahakama na wao ndio magereza,
tutawaagiza viongozi wetu katika halmashauri zinazoongozwa na CUF
kukataa kauli na matamko ya namna hiyo.
“JUVICUF
tunakitaka Chama cha CUF kuwaagiza viongozi wake katika halmashauri
tunazoziongoza kwamba waache mara moja kutekeleza maagizo yasiyo na tija
kutoka kwa viongozi waliolewa madaraka.
“Tunawasihi
vijana waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila kujali
matamko yanayotolewa na viongozi waliolewa madaraka na kujifanya miungu
watu,” alisema.
Dahlia
alitolea mfano wa agizo lililotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwakamata wananchi wasiokuwa na kazi
maalumu ambapo alisema hayo ni miongoni mwa maagizo ya ovyo na hayapaswi
kutekelezwa.
Kiongozi
huyo wa vijana alisema agizo hilo ni kinyume cha sheria huku
akitahadharisha kuwa utekelezaji wake utahusisha askari kupiga watu,
visa na vijana kubambikiwa kesi zisizokuwa na sababu.
“Ni
ajabu sana na hii haipo kote duniani kibali cha kuwakaguwa wananchi
majumbani kutolewa na viongozi wa kisiasa, mahakama zina kazi gani?
serikali imefanya maisha kuwa magumu na ajira kuwa ngumu kupatikana
halafu wao wanaibuka na sera ya kukamata watu wasio na ajira,” alisema Dahlia.
0 comments:
Post a Comment