Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>HUU NI UTABIRI WA MOURINHO BAADA YA POGBA KUTUA OLD TRAFFORD.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anaamini kwamba timu yake
itarejesha kiasi cha fedha baada ya kuvunja rekodi ya usajili wa dunia
kwa kumsajili Paul Pogba, huku akisisitiza kwamba nyota huyo ana miaka
takriban kumi mbele ya kung’aa.
Pogba amekamilisha uhamisho wake wa euro mil 110 kurudi United akitokea kwa kibibi kizee cha Turin Jeventus mapema leo asubuhi.
“Ana nafasi ya kuwa moyoni mwa mashabiki wa klabu hii kwa miaka kumi na zadi,” Mourinho amesema.
“Paul ni moja ya wachezaji bora duniani na atakuwa mchezaji muhimu
sana kwenye kikosi cha United na nataka nimfanye awe tegemeo kubwa kwa
siku za usoni.”
“Ana kasi, nguvu, anafunga na ana uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo vizuri kuliko wachezaji wengi ambao wamemzidi umri.”
“Kwa umri wake wa miaka 23, ana nafasi ya kujimilikisha nafasi yake
kwa miaka mingi zaidi. Bado ni kijana ataendelea kuimarika zaidi.”
Pogba amedumu Juventus kwa miaka minne, ameshinda ubingwa wa Serie A
kwa miaka yote minne. Mourinho anaamini Mfaransa huyo atahamishia makali
yake kunako Old Trafford na kurejesha heshima ya Man United iliyopotea
kwa tangu msimu wa 2012-13.
Related Posts:
#MICHEZO>>>Timu za Azam na Simba zaiyakikishia ubingwa Timu ya Yanga.Fahamu zaidi hapa.
Matokeo ya sare kati ya Simba dhidi ya Azam yanaifaidisha Yanga
ambayo imeendelea kukaa kileleni mwa ligi bila presha kubwa kutoka kwa
Simba na Azam ambazo zimeshindwa kupata matokeo ya ushindi ili
kuisogelea Yanga kilel… Read More
#MICHEZO>>>>>WAKATI SIMBA IKIBANWA NA AZAM, MWINYI KAZIMOTO ALIKUWA AKISHEREKEA NDOA.Fahamu zaidi hapa.
Kiungo mkongwe wa wekundu wa Msimbazi Simba Mwinyi Kazimoto, hakuwepo
kwenye kwenye kikosi cha Simba kilichocheza dhidi ya Azam FC kwenye
mchezo wa ligi kutokana na kuwa mapumzikoni kufuatia kufunga ndoa
Jumamosi April 3… Read More
#MICHEZO>>>HATIMAYE KOCHA WA ARSENAL ..ARSENE WENGER AKUBALI YAISHE KWA MASHABIKI.Fahamu zaidi hapa.
Wakati shinikizo la kutakiwa kuondoka likiendelea kupamba moto katika
mitaa mbali mbali ya kaskazini mwa jijini London, meneja wa klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger amesalimu amri kwa kukubaliana na hali halisi.
Wenger amb… Read More
#MICHEZO>>>Manchester unite yaipunguzia kasi ya kutangaza ubingwa wa Ligi ya Uingeleza Leicester.Fahamu zaidi hapa.
Manchester United (4-1-4-1): De Gea 6.5; Valencia
6.5, Smalling 6.5, Blind 6, Rojo 5; Carrick 7; Lingard 5 (Mata 61mins),
Rooney 7.5, Fellaini 5 (Herrera 74), Martial 7,5; Rashford 6 (Depay 82)
Subs (not used): Ro… Read More
VIDEO>>>KAMA HUKUIONA MECHI YA SIMBA NA AZAM BASI HII HAPA.
Ligi kuu Tanzania (VPL) iliendelea jana, pale uwanja wa taifa
palichimbika mechi kubwa kati ya SIMBA SC wakitoshana nguvu na AZAM FC
na matokeo hadi kipyenga cha mwisho ni suluhu. Hebu cheki kosa-kosa hizo
hapo. Picha za … Read More
0 comments:
Post a Comment