Kuna kila dalili, Simba itataka kumlinda mchezaji wake Ibrahim Ajibu asipate kadi ya tatu ya njano.
Ajibu
ana kadi mbili za njano na benchi la ufundi la Simba, linaweza
kujithatiti asijeze mechi ijayo dhidi ya Majimaji ili kuhakikisha
anaivaa Yanga Oktoba Mosi.
“Kweli
Ajibu ana kadi mbili za njano na sisi watu wa benchi la ufundi
tumeliona hili. Lakini bado utabaki kuwa uamuzi wa kocha mwenyewe
(Omog),” kilieleza chanzo.
Simba inaivaa Majimaji Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo Simba watakuwa kwenye maandalizi ya mechi yao dhidi ya watani wao Yanga, Jumapili inayofuatia.
Hivyo
suala la tahadhari linaweza kufanya Ajibu akose mechi hiyo ili
kuhakikisha anakuwepo kusaidia safu ya ushambulizi dhidi ya Yanga.
0 comments:
Post a Comment