Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho kwa
viwanja sita ambako kwa mara ya kwanza timu zote za Dar es Salaam
zitakuwa mikoani kupambana kutafuta nafasi bora katika ligi hiyo
iliyoanza Agosti 20, 2016 kabla kufifikia ukomo wa mzunguko wa 15,
Novemba 12, mwaka huu.
Vinara
ligi hiyo kwenye msimamo msimu wa 2016/17, Simba SC watakuwa wageni wa
Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati mabingwa watetezi wa
taji hilo Young Africans itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Africans
Lyon pia ya Dar es Salaam itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting
kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati Maafande wengine kutokea
mkoani humo – JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye
Uwanja wa Majimaji ilihali Ndanda itawakabiri Ndanda FC kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ligi
hiyo itaendelea Alhamisi Novemba 3, mwaka huu kwa michezo miwili ambayo
itafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Mwadui kuialika Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa Mwadui Complex huko Shinyanga huku Mbao Fc ikiwa na
kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,
jijini Mwanza.
Wakati
ligi hii ikiingia ukiongoni kwa nusu msimu, TFF inatoa wito kwa timu
kuajiandaa na dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuanza Novemba 15,
mwaka huu kusajili wachezaji mahiri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mwendelezo wa ligi hiyo nusu ya msimu uliobaki utakaoanza baadaye
Desemba.
Wakati
wa usajili wa dirisha dogo ndipo michuano ya hatua ya awali ya kuwania
Kombe la Shirikisho la Azam 2016/2017 inatarajiwa kuanza Novemba 19,
mwaka huu ambako pia imepangwa kuzindua michuano hiyo hukop mkoani Mara.
Safari
hii timu shiriki zimeongezwa mabingwa wa mikoawa mwaka jana hivyo
kufikisha idadi itakayofika 86 badala ya 64 za msimu ulioipita.
Imechukuliwa mikoa 22 baada ya ile mitano, kupanda Daraja kucheza Ligi
Daraja la Pili msimu huu ambayo imeanza kushika kasi.
0 comments:
Post a Comment