Wabunge wawili wa CCM na Chadema wametaka Bunge liahirishne shughuli
zake mara moja na kutoa nafasi kwa wabunge kujadili suala la utekwaji wa
raia nchini.
Wabunge hao ni Hussein Bashe(Nzega Mjini) na Joseph Mbilinyi(Mbeya
Mjini)wameomba mwongozo wa Spika kuhusu suala hilo leo asubuhi.
Bashe amesema ni muhimu suala hilo likajadiliwa kwani iko orodha ya wabunge 11 akiwemo yeye mwenyewe wameambiwa wakae chonjo.
Bashe alisimama kwa kutumia kanuni ya 47 vifungu (i,ii,iii) akamtaka
Naibu Spika kusimamisha shughuli za bunge kwani jambo lililombele yao ni
kubwa na likiachwa linaweza kuwa na madhara makubwa na kuichafua
taswira nzima ya serikali.
Hoja ya mbunge huyo iliungwa mkono na Mbilinyi ambaye amesema kuwa Taifa
limekuwa gizani kutokana na utamaduni wa utekaji ambao tangu mwanzo
haukuwepo na akamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
kujihuzulu mara moja nafasi yake ili kulinda heshima.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment