Msanii wa bongo fleva Nuh Mziwanda amesema Shilole ni msanii mwenzake na
walivyoenda Zanzibar hawakuwa pamoja kila mtu alikuwa ameenda kwa kazi
yake.
Akipiga story kupitia eNewz ya EATV Nuh Mziwanda amesema hata kama
akiamua kutoka nje ya ndoa siyo lazima atoke na Shilole kwakuwa wanawake
ni wengi na anapokuwa kwenye show huwa anakutana na wanawake wengi
hivyo siyo lazima atembee na Shilole..
Hata hivyo Nuh Mziwanda amesema haoni sababu ya kutoka nje ya ndoa yake
na mashabiki zake wanapaswa kuelewa kwamba anapokuwa kwenye show moja na
Shilole ni kutokana na maslahi hawezi kukataa pesa eti kwa sababu show
aliyopata Shilole yupo.
Pia Nuh alimalizia kwa kusema "Zanzibar kila mtu alienda kwa kazi zake
japo tulijikuta tumeshukia hotel moja, Shilole akiwa ameenda kuzindua
Pub lakini mimi nilikuwa nimeitwa na nimepewa pesa zangu kwa ajili ya
kufanya show"
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment