Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake leo
Alhamisi kwenda Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger.
Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka Alhamisi
jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.
Wachezaji watakaondoka ni Makipa: Deogratius Munishi na Beno Kakolanya.
Nafasi ya ulinzi: Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vicent Bossou , Juma Abdul ,
Vicent Andrew, Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin
Yondani.
Viungo: Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke, Said Makapu,
Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.
Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine
Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey
Chirwa na Yusuph Mhilu.
Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano
Young Africans SC
12/04/2017.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment