Elizabeth Michael (Lulu) amedai ndoa yake na mpenzi wake Dj Majay
inakaribia.Muigizaji huyo ambaye ameonekana kutulia sana tangu alipokuwa
na mahusiano na bosi huyo wa EFM na TVE amesema hivi karibuni wale
waliokuwa wakitaka waachane watabaki midomo wazi.
“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo
wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana
natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,” ameliambia gazeti la
Mtanzania.
Lulu ameongeza kuwa anatamani kuwa mke bora kwenye ndoa yake kama alivyokuwa sasa kwenye mahusiano yake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment