Kila siku huwa tunapenda kuwaambia wanawake ni warembo. Neno hili
limewaingia katika akili zao kiasi cha kuwa ile maana msingi ya neno
‘wewe ni mrembo’ imepotea. Hii ni kwa sababu baadhi ya wanaume wasiojua
kutongoza wanaishia kulitumia neno hili vibaya kiasi cha kuwa neno hili
limepoteza uhalisia.
Ok, tukiachana na hayo, je ulikuwa wajua kuwa wanawake hupenda kusifiwa?
Na ulikuwa ukijua kuwa kumsifia mwanamke mara kwa mara ni njia moja
wapo ya kutongoza? Well, leo tumekuja na mambo tofauti ambayo unapaswa
kutumia ili umshawishi mwanamke kuwa ni mrembo, na wala hataona kama ni
maneno unalompakizia ama maneno ambayo ameyazoea kuyaskiliza awali...
Zama nami...
Jambo la #1
Wakati unapotaka kumsifia mwanamke kuwa ni mrembo, usimwambia, “Wewe ni
mrembo” mara kwa mara kwa sababu itafikia mahali flani neno hilo
litaisha ladha. Badala yake tafuta sehemu muhimu kutoka kwa mwili wake
ambayo utaitumia kama kigezo cha kumsifia. Kwa mfano kama umependezwa na
pua yake mwambia, “Nimependezwa na pua yako, kila mara nikiiona
najiskia na furaha.” Ama kama umependezwa na mashavu yake unaweza
kumwambia, “Mashavu yako ndio nuru ya macho yangu, yanapendeza.”
Kumwambia mwanamke maneno kama haya yatamfanya atamani kuwa kando yako.
Pia ataona kuwa unamwona anapendeza, unamakinika kuuona urembo wake
kupitia kwa viungo vyake vya mwili.
Jambo la #2
Kumsifia mwanamke urembo wake hakuhusishi ngozi yake ya nje pekee, bali
pia sehemu yake ya ndani, yaani nafsi yake. Wanaume wengi huwa
wanamakinika kumsifia mwanamke umbo, sura na shepu yake huku wakisahau
kuwa nafsi ya mwanamke ina umuhimu. Kumsifia mwanamke kwa ujasiri wake,
ubunifu wake, hikma, na ujanja kutakupa mkono wa mbele zaidi wakati
unapomtongoza ama unapomshawishi. Jambo hili tulishawahi kulizungumzia
katika moja ya hatua ya kumtongoza mwanamke ambaye hayuko ligi sawa na
wewe. Kumshawishi na kumsifia mwanamke nafsi yake kutamfanya
ajiunganishe na wewe zaidi kuliko mwanamke yeyote yule, hivyo hatua iko
kwako sasa.
Jambo la #3
Unapomsifia mwanamke usitumie maneno yayo kwa hayo. Yaani wewe kila siku
ukikutana na yeye unamwambia, “Nakupenda, leo umeangaza nafsi yangu.”
Matumizi ya neno moja siku nenda siku rudi kutamfanya mwanamke atilie
shaka iwapo unasema maneno hayo ndani ya moyo wako ama unasema
kumridhisha tu. Well, mbona usije na misamiati mipya? Ama mbona usije na
maneno ambayo angetamani kuyaskia? Ukitumia maneno kama ‘hurulaini’,
‘malkia, leo nimekuja kwa milki yako’, ‘ua langu la waridi’ nk
kutamfanya mwanamke akupende zaidi na zaidi. So anza kutafuta maneno
ambayo anayapenda. Usiingiwe na uvivu wa kutumia maneno yayo kwa yayo.
Kumbuka hapa unataka kuwa mbora zaidi kati ya wanaume wale wengine.
Chukua hatua sasa.
Jambo la #4
Wakati ambapo umeamua kumsifia mwanamke kama huyu, hakikisha kuwa
unamwangalia machoni. Kama ni mwanamke ambaye ndio unaanza kumfukuzia
basi jenga confidence ya kumwangalia machoni. Usimsifie huku ukiangalia
pembeni ama kuangalia kando. Kumbuka wewe ni Mwanaume Alpha, na wanaume
alpha huwa hawatatiziki kama wanatoa hisia zao kuhusu wanawake
wanaowapenda.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment