kila mtu huwa anajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa mafuta tumboni, iwe
tumbo ni la kati au ni kitambi kimejitokeza. Kwa mwili mnene wenye
mafuta mengi ni vigumu kuona matokeo mazuri ya kuridhisha kwa kufanya
mazoezi pekee, maana asilimia hamsini ya mafuta mwilini huifadhiwa chini
ya ngozi, na kiasi kingine kilicho baki huwa ndani ya misuli. Kufanya
mazoezi ya mwili pekee hakuwezi kuondoa mafuta hayo mwilini.
Mtu mnene akifanya mazoezi ya kuvuta tumbo hawezi kuona matokeo, hata
kama akirudia mazoezi hayo mara mamia kwa siku, kitakachotokea ni kweli
ataimalisha misuli yake ya tumbo ila hatoweza kuona matokeo hayo kwa
sababu tumbo bado litakuwa limezungukwa na mafuta.
JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA
Kuna usemi unaosema, kwa matokeo ya mazoezi unahitaji.. “ASILIMIA 70
DAYATI, ASILIMIA 30 ZOEZI!”. Kwa matokeo mazuri na ya haraka njia hii
hutoa matokeo mazuri Zaidi tofauti na kupiga mazoezi pekee ambapo ni
kweli unaweza kuwa unaumguza mafuta mwilini ila hauwezi kuunguza mafuta
yakutosheleza kwa siku kuweza kuonyesha matokeo mazuri ya mazoezi
unayopiga.
Ila kwa njia ambayo itakupa matokeo ya muda mrefu maara nyingi huwa ni
ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, na matokeo haya nayaita ya muda mrefu
maana mazoezi hayo yatakufanya uwe na adabu ya kubadilisha mwenendo wa
maisha yako na kuutunza mwili wako kwa heshima.
Njia ya 70 kwa 30 inatoa matokeo mazuri maana asilimia 70 ya upunguaji
wa mafuta mwilini hufanywa na dayati ya kuangalia nini cha kula na kipi
cha kuondoa kabisa kwenye mlo wako wa kila siku. Hata hivyo kwa
kuangalia dayati pekee haiwezi kukupa matokeo mazuri, maana tafiti mbali
mbali za kisayansi juu ya kupunguza mafuta mwilini zimeonyesha huwezi
kupunguza mafuta mwilini kwa dayati pekee na kupata mwili wa kuvutia
pasipo kufanya aina yeyote ya mazoezi ya mwili, ukitaka mwili uliopungua
kwa mpangilio na mvuto lazima uhusishe pia mazoezi ya mwili.
Njia kuu ya kupunguza mafuta kwa njia ya dayati ni kupangilia milo yako
ya siku, iwapo ukitaka kujua ni chakula gani kitakachokupa matokeo
mazuri
Lazima ujue mlo wako utaupangilia katika hali gani, kwa mfano badala ya
kula ovyo hovyo, unatakiwa upangilie milo yako kwa kula kiasi, kama
umezoea kujaza tumbo wakati wa kula, jaribu kushusha mlo wako uwe
unakula kwa kuondoa njaa kwa kuupa mwili vile virutubisho unavyovihitaji
tu, na unaweza kula milo mitatu mpaka mitano kwa siku na usizidishe
zaidi ya hapo.
Hakikisha unakula mlo kamili ila kwa kuhakikisha huli vyakula
vilivyotengenezwa kwa sukari, na zingatia kuachana na milo
inayotayarishwa kwa haraka, (fast sood) kama chipsi, vitafunwa na
vinginevyo vinavyohusiana na hivyo, zingatia kula vyakula vyenye protini
na milo yako iwe kamili na hasa pendelea kula mboga mboga.
Kwa kuzingatia dayati na kwa kufanya mazoezi yanayohusisha kuchemsha
mwili wako kwa kuongeza mapigo ya moyo zaidi utafanya mwili wako
ubadilike na kupata matokeo unayo yahitaji, maana kwa kadri mwili wako
unavyochemka ndivyo unavyozidi kuchoma mafuta mwilini, na kwa jinsi
mwili wako unavyopunguza mafuta utafanya ngozi yako kukakamaa na kufanya
mwili wako kupata shepu, kwa hiyo kitu cha kufanya ni kukazania mazoezi
yanayoongeza mapigo ya moyo na kusababisha upumuaji wa haraka, fanya
mazoezi hayo mara tano kwa wiki
Mazoezi yote unayofanya hakikisha yanahusisha sehemu zote za mwili
kuanzia misuli ya mikono, nyonga, mgongo, mapaja, misuli ya chini ya
miguu na sehemu zote za mwili kwa ujumla.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment