JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa
Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa
kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa
mapenzi maeneo ya Kibamba.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro
amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo
mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya
kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine
ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.
Alieleza
kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji
aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu
(sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;
“Nendeni
mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema
upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani.
Katika
hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia watatu wa kigeni kutoka
Afrika Kusini wakiwa na vipande viwili vya meno ya vinavyokadiriwa kuwa
na uzito wa kilogramu 45 na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao
walikamatwa Machi 28 mwaka huu maeneo ya Upanga Dar.
Sirro
ameeleza kuwa upelelezi juu ya watuhumiwa hao bado unaendelea ili
kubaini kama walikuwa wanamiliki nyara hizo za serikali kihalali na
mawasiliano kati ya Idara Maliasili yanaendelea.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment