Mbunge
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Jaku Hashimu Ayoub ametaka
makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali za Serikali yapelekwe Zanzibar ili
kulipia deni la umeme.
Jaku
alisema hayo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, ambapo
alisema kuna kodi zinazolipwa Tanzania Bara, lakini hazipelekwi Zanzibar
kwa ajili ya kusaidia maendeleo ikiwamo kulipia deni hilo.
Mbunge
aliyedai kuwa na ushahidi juu ya kauli yake hiyo na kwamba yupo tayari
kuutoa, alisema fedha hizo ni muhimu zikapelekwa ili zisaidie ulipaji wa
malimbikizo ya deni la umeme.
Machi
9, mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilitangaza kuikatia
umeme Zanzibar kutokana na limbikizo la deni la zaidi ya Sh275.38
bilioni.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema wameipa siku 14
kuhakikisha kuwa inalipa deni hilo. Hata hivyo, siku chache baadaye
Tanesco ilitangaza kulipwa Sh10 bilioni kama malipo ya awali ili isikate
umeme visiwani humo.
Awali,
katika swali la msingi, Mbunge wa Magomeni (CCM), Jamal Kassim Ali
alitaka kujua iwapo Serikali haioni haja ya kodi ya mishahara (paye) kwa
wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) isikusanywe
visiwani humo kwa ajili ya kusukuma maendeleo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji alisema kwa mujibu wa
Sheria ya Mapato sura ya 66, kifungu cha 4(a) na (b), kodi za kampuni ni
za Muungano na zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia, alisema hata kampuni ambazo zimesajiliwa Tanzania Bara lakini zinafanya kazi Zanzibar, kodi zake zinakusanywa Bara.
Naibu
waziri alisema iwapo kampuni itakuwa imesajiliwa Zanzibar na ikawa na
matawi Tanzania Bara inatakiwa kulipa kodi yake Zanzibar.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment