Mbuge wa Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu amefunguka na kusema kuwa
wasaidizi wa Rais wakiwemo wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
mawaziri, na wabunge wa upinzani na washauri wa karibu wa Rais wamekuwa
wanafiki na kushindwa kumshauri
Dalaly ametoa kauli hiyo kwa madai ya kushindwa kumshauri vizuri Rais
Magufuli katika mambo ya msingi ambayo yanaweza kuleta maendeleo katika
taifa
Dkt. Kafumu amesema hayo bungeni wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu, mbunge huyo anasema viongozi hao wanashindwa kutumia vyema
sifa kuu tatu za Rais Magufuli ambazo ndizo zilikuwa zinahitajika kwa
muda mrefu.
"Tumepata Rais ambaye sifa zake tatu zilikuwa zinahitajika sana, sifa ya
kwanza ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa wanyonge, sifa ya pili
anaamua papo kwa papo hacheleweshi, sifa ya tatu anataka watu wafanye
kazi, sifa hizi sisi baadhi yetu tumezitumia vibaya tumeshindwa
kuzitumia vyema ili nchi yetu isonge mbele. Baadhi yetu wabunge wa
upinzani na CCM, baadhi yetu mawaziri siyo wote na baadhi yetu wasaidizi
wa Rais tumeshindwa kusema kweli, tumeshindwa kushauri kwa ukweli
tumekuwa wanafiki na hili jambo litatuua sana" alisema Kafumu
Kafumu anadai wengi wao wamekuwa wakitengeneza ushauri nusu nusu kwa
Rais jambo ambalo linafanya zile sifa zake tatu kuu zitumike vibaya, kwa
kufanya maamuzi kwenye jambo ambalo huenda halijakamilika.
"Rais anaamua pale pale unafikiri kitatokea nini? tunahitaji uchambue
ushauri wako, uupime, uutengeneze ushauri uende umekamilika, na Rais
wetu huyu anayefanya papo kwa papo akiamua nchi inasonga mbele, sasa
hivi haya yote tunayoyaona ni kwa sababu ya unafiki umezidi miongoni
mwetu" alisema Kafumu
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment