Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa wastani wa 1.4 kutoka
asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Februari hadi asilimia 6.4 kwa mujibu wa
taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya sababu zilizochangia ongezeko hilo
ni kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula ambapo
vyakula vilivyopanda bei ni pamoja na mchele, sukari, unga wa mahindi,
mtama, ndizi pamoja na mihogo mibichi.
Kufuatia ongezeko hilo, baadhi ya wakazi Jijini Dar es Salaam wametoa
maoni yao na kutaja ukosefu wa kipato kuwa unaongeza ugumu wa maisha
hasa kwa wafanyabiashara ambao wamelalamikia upungufu wa wateja sambamba
na ushauri wa hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment