MKUU
wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani Majid Mwanga, amesema nyumba zaidi
ya nyumba 100 zilizopo Kata za Bwilingu eneo la Chalinze Mzee na Msoga
zimeharibika na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha.
Mvua hizo zimeathiri baadhi ya maeneo ya Msoga, Chalinze Mzee, darasa moja katika Shule ya Msingi Kidogozero, Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.
Akizungumza na wananchi waliopatwa na athari hizo, baada ya kutembelea maeneo hayo, Mwanga alisema kwa sasa majirani, ndugu wanaendelea kusaidiana.
“Serikali inatafakari cha kufanya kutafuta wadau, ila lazima muhakikishe ndugu zangu mnasaidiana wenyewe kwa wenyewe pasipo kuitegemea Serikali pekee.
“Nashukuru hakuna maafa makubwa makubwa wala ya vifo na majeruhi zaidi ya kubomoka kwa nyumba na kuharibika na sasa tunafanya kila linalowezekana ili kuweza kuwapa msaada wa kibinadamu unatakiwa,” alisema Mwanga
Baadhi ya wakazi waliathirika na mvua hizo akiwemo Rashid Mwinyigoha, alisema mvua hiyo ni kubwa na haijawahi kutokea katika eneo hilo na hata kuwasababishia hasara.
Alisema hali yao ni mbaya kwani nguo, fedha, chakula vimesombwa na maji na sasa hawana la kufanya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bwilingu, Lucas Rufunga (CCM), alisema wameanza kufanya tathmini ya awali kwa kupita nyumba kwa nyumba ili kubaini hasara waliyoipata wananchi wake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment