Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
amewaapisha viongozi aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali.
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Magufuli amemuapishwa Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Prof. Kitila Alexander Mkumbo ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Dkt. Ave Maria Emilius Semakafu ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mhe. Baraka Haran Luvanda ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India.
Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu
katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es
salaam April 5,2017
Bw. Charles Edward Kichere ameapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Aidha,
Viongozi hao wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma
kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Bw. Waziri Yahaya Kipacha.
Akizungumza
baada ya kuapishwa kwa viongozi hao, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan amewapongeza kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo na amewataka
kufanya kazi kwa kutanguliza maslai ya Taifa na kwa kuzingatia sheria na
taratibu zilizowekwa.
“Tutawapa
ushirikiano wote mtakaouhitaji ili kufanikisha kazi zenu lakini na
nyinyi msituangushe, Bw. Kichere tunakutegemea ukaimarishe ukusanyaji wa
mapato pale TRA na pia ukawaambie maafisa wako na mameneja wa mikoa
waache kutoa kauli za kuigombanisha Serikali na wafanyabiashara,
wakusanye kodi kwa kufuata sheria na taratibu na pia wawe na lugha
nzuri.
“Prof.
Kitila Mkumbo tunategemea utaongeza msukumo kutatua matatizo ya maji,
utasaidia kufanikisha kampeni ya kumtua Mama ndoo ya maji, Watanzania
wapate maji safi na salama” amesema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment