Home »
Burudani
» #BURUDANI>>>>MOROGORO IMOOO!!,KESHO TIGO FIESTA NDANI YA JAMHURI STADIUM.FAHAMU ZAIDI HAPA.
WASANII 18
wa muziki wa Bongofleva watapanda jukwaa moja kwenye tamasha la Tigo
Fiesta litakalofanyika kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Wasanii hao watatoa burudani kwenye
tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya Tigo ambalo linafanyika
katika mikoa mbalimbali nchini.
Nyota hao wanaotarajiwa kutoa burudani
katika tamasha hilo ni pamoja na Ben Pol, Christian Bella, Jux, Nandi,
Mr Blue, Chege,Dully Sykes, Fid Q na Darassa.
Wengine ni Linah, Vanessa Mdee, Mau,
Moni,Snura, Man Fongo, Baraka Da Prince, Bonge la Nyau pamoja na kundi
la Weusi linaloongozwa Joe Makini.
Tamasha la Tigo Fiesta litafanyika
katika mikoa 15 ambapo tayari limefanyika katika mikoa mitano ya Mwanza,
Kagera, Shinyanga, Singida na Dodoma.
0 comments:
Post a Comment