Friday 21 October 2016

#YALIYOJIRI>>>>>HUYU NDO baba mzazi aliyemchoma mtoto wake sindano na kumwambukiza UKIMWI kwa makusudi.Fahamu zaidi hapa.

Bryan Jackson, mtoto aliyechomwa sindano iliyokuwa na damu yenye virusi vya HIV na Baba yake akiwa mchanga, huku baba huyo akiwa na matumaini kwamba hatamuona akikuwa na kwamba atafariki.

Hakuna mtu aliwahi kudhani kwamba miaka 24 baadaye Stewart Jackson (Baba wa mtoto huyo), atakabiliana na mwanawe mahakamani katika kesi ya unyama huo aliyoufanya. Wawili hao walikutana mahakamani licha ya kutoonana tangu Bryan alipokuwa mtoto.

Yote haya yalianza wakati mamake na babake walipokutana katika kambi moja ya kijeshi mjini Missouri ambapo wote walikuwa wakijifunza utabibu. Waliishi pamoja na miezi mitano baadaye kati kati ya mwaka 1991 mamake alipata ujauzito.
 Familia ya Jackson – Stewart Jackson na mwanawe Bryan kulia 

Simulizi ya Bryan Jackson ambaye kwa sasa ni ‘Motivational Speaker’:
‘Wakati nilipozaliwa baba yngu alikuwa ni mwenye furaha tele, lakini kila kitu kikabadilika alipoenda katika operesheni ya Desert Storm. Alirudi kutoka Saudia akiwa na mawazo tofauti sana kuhusu mie’,alisema Jackson.

Baba yake alianza kukataa kwamba Jackson ni mwanae, huku akitaka kufanyiwa uchunguzi wa vinasaba vya DNA ufanyike na pia akaanza kumtusi mama yake ambayo ikapelekea wawili hao kutengana.

Wakati alipoachana na mamake, wazazi hao walisumbuana sana kuhusu mahitaji ya mtoto , ambayo Stewart alikataa kulipa na mara nyengine wakati wa wakigombana  alimtishia mama yake Jackson.

Alikuwa akitoa matamshi makali kama :Mwanao hataishi zaidi ya miaka mitano, na nitakapoachana nawe sitawachia chochote kinachotuunganisha.

Wakati huohuo Stewart ambaye alipata kazi kama mkaguzi wa damu katika maabara moja, alianza kwa siri kuchukua violezi vya damu yenye maambukizi nyumbani,wachunguzi baadaye walibaini.

”Alikuwa akifanya utani na rafiki zake akisema: Iwapo ningetaka kumwambukiza mtu na virusi hivi, hakuna mtu angejua ni nini kimetokea au ni nani amemuathiri, alisema Jackson.

Wakati Jackson alipokuwa na miezi 11, mama yake na baba yake walikuwa hawawasiliani, lakini wakati Jackson alipolazwa hospitali kwa kuugua pumu, mama yake ilimbidi ashike simu na kumpigia baba yake.
Bryan na mamake
 
Mama yangu alimpigia simu kumuelezea, alidhani angetaka kujua kama mwanae ni mgonjwa. Alipopiga simu rafiki zake walipokea simu na kusema kuwa Stewart hana mtoto.

Siku ambayo Bryan alikuwa atolewa hospitalini, Stewart  alimtembelea hospitalini. ‘Baba yangu alimtuma mama yangu katika mkahawa mmoja ili kununua kinywaji ili aweze kubakia nami’. Alipoona hakuna mtu karibu, Stewart alichukua damu iliyo na maambukizi ya UKIMWIna kunidunga nayo’.

Mama aliporudi alikuta natapatapa kitandani huku damu zikitoka mwilini na ndipo alipoita madaktari na manesi wakaja kunisaidia. Huku wakisema damu iliyoingizwa mwilini mwangu haikufanana na aina damu yangu na hivyo nikatulizwa. Stewart alikufanya hivyo huku akitegemea ningefariki ili asilipe mahitaji ya mtoto kamwe”, alisema Bryan.

Baada ya hapo maisha yangu yakawa ni ya hospitalini tu kila kukicha, mafanikio yoyote. na baada ya muda ndipo moja ya madaktari walikuwa wakinitibu aliombwa nipimwe kipimo chenye kubaini virusi vya UKIMWI na kwa bahati mbaya majibu yalitoka Chanya (Positive) na pamoja na magonjwa nyemelezi manne.

Bryan aliishi kwa tabu sana kutokana na unyanyapaa uliyokuwepo zamani kuhusu watu wenye maambukizi ya UKIMWI. Shuleni ilikua zaidi kwani watu walikuwa akifikiri mtu anaweza kupata gonjwa hilo hata kwa kutumia choo kimoja na mwathirika.

Bryan kwa sasa ana umri wa 24, na anaendelea kuishi na virushi vya UKIMWI, mwenyewe anasema anashukuru kwani alikua ni mtu wa kunywa vidonge 23 kwa siku mpaka sasa anakunywa kidonge kimoja tu, CD4 zake zinamtosha. Ni kama amepona lakini ndo hivyo tena, ukiugua UKIMWI we ni mgonjwa wa UKIMWI milele hakuna kupona moja kwa moja, japokuwa uwezo wa kumwambukiza mtu mwingine ndio unaopungua.

0 comments:

Post a Comment