Friday 21 October 2016

#YALIYOJIRI>>>>WANAOKULA CHAKULA KIBICHI WAKO HATARINI KUPATA KICHOCHO, MINYOO NA MATENDE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Watu milioni 47 nchini wapo katika hatari ya kupata magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele yakiwemo Minyoo,Matende na Kichocho, Aidha watu milioni 12.5 wapo hatarini kupata ugonjwa wa Trakoma huku milioni 4 wakiwa hatarini kupata ugonjwa wa Usubi.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Ofisa mpango wa kudhibiti magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele(NTD), Oscar Kaitaba kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.

Kaitaba amesema kuwa katika wagonjwa milioni 47 waliopo hatarini kupata matende, kichocho na minyoo, watu ambao wapo hatarini kupata ugonjwa wa minyoo ni wale ambao wanakula chakula ambacho hakijaiva.

Kaitaba ameongeza kuwa katika mpango wa kudhibiti magonjwa hayo, Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu katika mkoa wa Dar es Salaam kutakuwa na ugawaji wa dawa za kingatiba za Minyoo ya tumbo ,matende na mabusha ambazo zitatolewa katika vituo maalum vilivyoteuliwa.

“Vituo hivyo ni pamoja na Stendi za mabasi , masoko, hospitali, ofisi za serikali za mitaa, ofisi za Wizara, taasisi na kambi za jeshi na magereza,”alisema Kaitaba.

Alitaja aina za dawa kinga ambazo zitatolewa kuwa ni Albendazole na Ivermectim na kwamba walengwa ni wananchi wote kuanzia miaka mitano na kuendelea isipokuwa wajawazito na watu ambao ni wagonjwa mahututi. Aidha Kaitaba alisema wanatarajia kufanya upasuaji kwa watu 400 wenye mabusha katika manispaa ya Ilala ambao utafanyika katika Hospitali ya Pugu Kajiungeni hivi karibuni

0 comments:

Post a Comment