Monday 31 October 2016

#YALIYOJIRI>>>SMZ yatoa onyo kwa watakaoleta vurumai za kidini visiwani humo.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu amesema Zanzibar inahistoria ndefu ya uvumilivu wa kidini na kuonya kwamba Serikali itawakuchulia hatua wale wote watakaolete chokochoko za kidini.

Akizindua jimbo mpya za ibada za Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania, Waziri Gavu alisema kwamba tofauti za imani ya dini kamwe isiwe chanzo cha kuigawa jamii na mifarakano.

“Ndugu zangu waumini, tofauti za dini isiwe chanzo cha mifarakano katika jamii, tujiepushe na aina yoyote ya uchokozi au mgawanyiko, daima tuwe wamoja wenye kuheshimu imani za dini nyengine” Alisema Waziri Issa Gavu.

Waziri Gavu alisema kwamba ni jambo la aibu kuona watu wanagombana kwa sababu ya tofauti za imani za kidini. Aliwataka wananchi kuendelea kutunza amani na kuongeza upendo miongoni mwao.

Alisema Serikali itaendelea kuheshimu imani za dini na kwamba kila mwananchi anawajibu wa kufuata sheria na taratibu za nchi na kuonya kuwa Serikali haitochelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaovunja sheria za nchi.

Waziri Issa Gavu alisema kwamba Zanzibar ina historia ndefu ya uvumilivu wa kidini ambapo pia ina historia kongwe ya dini ya Uislamu na Ukristo.

Amewataka waumini wa kanisa hilo kuungana na waumini wengine katika kuhimiza umoja na mshikamano katika jamii na kusisitiza kwamba Watanzania wanawajibu wa kuishi kwa kuheshimiana, lakini pia kuvumiliana.

Katika hatua nyengine, Waziri huyo alisema Zanzibar imendelea kuwa sehemu tulivu na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuitunza amani iliyopo.

Waziri Gavu alisema kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka huu ulifanyika katika mazingira tulivu huku waumini wa dini mbalimbali wakiendelea na shughuli za ibada zao bila kusumbuliwa.

Katika uzinduzi huo, Waziri Issa Gavu amewahakikishia waumini wa kanisa hilo kwamba Serikali itanedelea kushirikiana nao ili kuona kwmaba kila muumini wa dini anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Na Dk. Juma Mohammed, Zanzibar

MWISHO

0 comments:

Post a Comment